Utukufu Wa Nyumba Ya Mwisho

(Hagai sura 2 msitari 9)

The glory of the latter house

Iwapo unataka kuchukua watoto wasio na wazazi kadhaa (hata kama ni mmoja) bila shaka shirika la kupeana watoto litakuja kwako nyumbani, wakuhoji wewe na mwenzako na waangalie mazingara yote, ilikuweka msingi kuwa mahali ambapo watoto wanaenda ni mahali ambapo wanaweza kupendwa na kutunzwa kwa njia yeyote ingawa chini ya ulinzi wako.

Iwapo huu ndio ungalifu tunachukua ilikuhakikisha kuwa, watoto wanaenda mahali pazuri kwa uwezekano kwa ajili yao, basi fikiria Mungu ataenda kuwa na uangalifu jinsi gani, kuhakikisha watu ambao wanavutwa makanisani mwetu katika wakati wa uvivio, wataenda mahali ambapo watapendwa, kutunzwa, kutiwa moyo na kupewa nafasi kukua katika kila sehemu ya maisha yao ambayo wanahitaji kuendelea.

Hebu tutazame nyuma katika kitabu cha Matendo tuone kama tunaweza kupata jinsi ambayo Mungu amekusudia kanisa lake kufanya kazi katika siku hizi za mwisho. Sura ya mwisho ya 2 kitabu cha Matendo msitari wa 42 kupitia mpaka mwisho inaonyesha kitu ambacho tunaenda kukiangalia sehemu kwa sehemu kwa kutafuta mpango halisi wa Mungu. "Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mtume. Nawote waliamini walikuwa mahali pamouja, na kuwa na vitu vyote shirika, waliuza mali zao na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawanyia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.

Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wanaokolewa."

Yesu aliongea mengi na wanafunzi wake, katika wakati mfupi alioweza kuwa nao, kabla ya kusulubishwa kwake, muda mwingi wa wakati huo ulitumika kuwafundisha mambo mengi. Aliweka mikononi mwao funguu nyingi, hakuna hata mmoja wao angewambia kwa uwazi jinsi wanaweza kuwa na mguzo mwema kwa jamii waliokuwa wanaishi kati yake.

Yohana sura ya 13 msitari wa 34 hadi 35 inatuambia kile Yesu aliwambia wanafunzi wake, baada ya kujinyenyekesha mwenyewe na kuwaosha miguu yao. "Amri mpya nawapa mpendane, kama vile niliovyowapenda ninyi, ninyi nani mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi."

Swali basi lafaa liulizwe "Yesu aliwapenda vipi wanafunzi wake?" Jibu ni rahisi sana ina weza kuhitimiswa kwa neno moja – kujitoa sadaka. Leo kwa sababu ya tamaa na kukosa kuamini kile ambacho bibilia inasema, ni vigumu kunena kuhusu utoajitoa sadaka.

Luka sura ya 6 msitari wa 38, ina nukuu mambo ambayo Yesu alinena sio kwa wanafunzi wake pekee, lakini kwa wote waliokata shauri kumfuata. "Wapeni watu vitu nanyi mtapewa, kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakacho wapa vifuani mwenu. Kwakuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakacho pimiwa."

Iwapo kweli watu waliamini hii, basi hakungekuwa na yeyote anayeishi katika umaskini katika kongamano la kanisa yeyote, na mataifa ambayo yanaendelea yataweza kuendelea katika hali ambazo ni heri, kuliko zile ambazo wanapitia kila siku. Katika Isaya sura ya 58 Mungu anaonyesha kitu ambacho anahitaji kutoka kwa watu wake.

Msitari wa 6 hadi 11 inasema: "Je, saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kizilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako?

Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapombazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia naye atasema, Mimi hapa, kama ukiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkujulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye Bwana, atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kiitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui."

Kuna magizo zaidi katika kifungu kiingine cha andiko, Mika sura ya 6 msitari wa 8 inasema: "Ee mwanadamu yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ilakutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako." Leo watu wengi huwasaidia wengine lakini wao kwanza, hii ni kinyume kabisa na upendo wa kujitoa ambao Yesu alionyesha ulimwengu.

Hebu tuangalie tena katika sura ya 4 ya kitabu cha Matendo, na tuchambue sehemu nyingine yake. Msitari wa 32 hadi 37 inasema kama ifuatavyo: "Na jamii ya watu wote walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni mali yake mwenyewe, bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi na neema nyingi ikawa juu yao wote.

Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta dhamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya avyohitaji. Na Yusufu aliye itwa na mitume Barnaba, (maana yake mwana wa faraja), mlawi asili yake ni mtu wa Kipro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume."

Hapa kuna mfano wa ajabu wa upendo wa kujitoa, unafikiri kanisa laweza kukushawishi kuuza shamba lako na uwape pesa ulizopata? Je, unaweza baki nalo lakini umwalike mtu aliye kwenye ushirika au anayetaka kujiunga na ushirika, aweze kuishi nyumbani mwako kwa muda usio julikana? Hili ndilo ambalo washirika wakanisa la kwanza walifanya. Nashangaa ni watu wangapi leo hii ambao wanaweza kuwa wakarimu hivyo.

Sehemu hii ya andiko inaanza na kauli ya ajabu, ya kuwa watu wote walikuwa na moyo moja na nia moja na mitume. Ni wapi ambapo twaweza kwenda leo hii na tupate kanisa ambalo laweza kusema hivi kuhusu kongamano lao? Kisha inatuambia mitume waliweza kushuhudia kwa nguvu nyingi ufufuo wa Bwana Yesu Kristo. Iwapo kanisa lingekuja katika umoja kama huu, ambaonwashilika walikuwa nao, basi ndipo ishara na miujiza zitatendeka katika kongamano la kusanyiko leo.

Matendo sura ya 2 msitariwa 42 hadi 47, inatuambia mambo mengine pia kuhusu kanisa la kwanza. "Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume.

Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kilamtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizindisha kanisa lika siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa."

Katika mwanzo wa kifungu hiki tunambiwa kuwa washilika waliendelea sana katika fundisho la mitume. Watu weng leo hutamani kama ingekuwa hivyo leo katika kiwango cha kanisa kote ulimwenguni. Kwa bahati mbaya watu wengi, viongozi wa makanisa pamoja na washilika wa kongamano lao wanaendelea kuvunja kanisa lao kwa kushidana kuhusu fundisho muhimu, kama vile kuzaliwa kwa Yesu na bikira, na iwapo kweli alikufa msalambani, au alizilai. Isipokuwa umeamini mafundisho sahihi ya bibilia katika masomo kama haya, utajipata wewe mwenyewe una hatia ambayo huwezi hata kujitetea mbele za Mungu katika siku ijayo ya hukumu.

Kwa sababu kila mtu alipokea fundisho la mitume, na kusanyiko lote walikuwa waminifu katika maombi na kukumbuka kifo cha Bwana, na ufufuo, kila siku kupitia kuumega mkate, miujiza mingi ilifanywa na mitume. Mwislamu aweza kuomba kama mara sita kila siku, je ushawahi kujaribu kufanya kiwango cha mshilika wa kongamano lako kuomba kama zaidi ya mara sita kwa mwezi? Iwapo umejaribu utajua jinsi hii ilivyo vigumu katika mengi ya makanisa, katika nchi za magharibi.

Sasa wacha tuende katika Matendo sura ya 6, mahali ambapo tutaangalia kifungu kingine, hata kama ni kifupi jinsi kilivyo ni muhimu. Msitari wa 1 hadi 8, inatuambia kuhusu watu wa kanisa la kwanza walikusanyika pamoja na mitume katika siku hizo. "Hata siku zile wanafunzi walipoku wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung’uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Wahebrania kwa sababu wajane wao walishahauliwa katika huduma ya kila siku. Wale thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. Basi ndugu wachagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile neno.

Neno hili likapendeza machoni pa makutano wote; wakamchagua Stefano mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikalao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.

Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile imani. Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kuibwa katika watu."

Wakati wanafunzi (sio kumi na wawili pekee) walianza kupeana mikate kwa wale waliokuwa katika kuhitaji, miujiza mikubwa ikaanza kufanyika, ykatika mikono ya wengine badala ya kumi na wawili pekee na idadi uyas wanafunzi ikaongezeka sana.

Labda jambo hilo hilo lingeweza kufanyika leo, iwapo mambo hayo yalifanyika katika jamii waliyoishi, na hili litawaweka huru wachungaji wetu na viongozi kuhubiri neno la Mungu kwa upana zaidi Watu hawa wengine walikuwa wa aina gani miongoni mwa mitume kumi na wawili? Maandiko hayajatuambia, lakini twaweza kufikiria kuwa makanisa wakati ule yalikuwa na utakatifu sana kuliko vile yalivyo leo, na watu waliokuwa ndani walikuwa na tabia ambayo ina mtukuza Mungu zaidi ya makanisa mengi ulimwenguni kote.

Paulo anaonyesha moja ya misingi ya mkristo, haijalishi ni mhuduma au ni mshilika wa kusanyiko. Hili linapatikana katika 1 Wakorintho sura ya 13 msitari wa 1 hadi 13, na inasema kama ifuatavyo: "Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

Tena nijabokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu ni ungue moto, kama sina upendo hainifaidii kitu.

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hahusudu; upendo hautakabali, haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha zitakoma, ya kiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; Lakini ijabo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatiliza mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa tunafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama vile nami ninavyojuliwa sana.

Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililokuu ni upendo." Inafaa ijulikane kuwa tafsiri nyingine zinatumia mapendo ijapokuwa kuwa tafsiri za kisasa zinatumia upendo.

Paulo aliandika zaidi kuhusu vile kanisa la kweli linastahili kuwa, na katika Waefeso sura ya 4 msitari wa 1 hadi 6 aliandika: "Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilifu mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha imani.

Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya wote na katika yote na ndani ya yote." Tena katika barua yake ya kwanza kwa kanisa la Korintho alionyesha jambo ambalo ni muhimu tena.

Katika 1 Wakorintho sura ya 12 msitari wa 1hadi 6 Paulo anaandika: "Basi ndugu zangu kwa habari ya karama za Roho, sitaki mkose ufahamu. Mwajua yakuwa mlipokuwa watu wa mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. Kwa hiyo na wahalirfu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.

Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;

Mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho huyo mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina ya lugha; na mwingine tafsiri za lugha. Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi zote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au tu huru; nasi zote tulinweshwa Roho mmoja.

Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. Mguu ukisema kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; Je! Si wa mwili kwa sababu hiyo. Na sikio likisema kwa kuwa mimi si jicho mimi si wa mwili, je! si la mwili kwa sababi hiyo? Kama mwili wote ukiwa jicho, kiwapi ukiusikia? Kama wote ni sikio kuwapi kunusa?

Bali Mungu ametia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa viungio ni vingi, ila mwili ni mmoja. Na jicho hali wezi kuuwambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja nanyi. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge vyahitajiwa zaidi. Na vile vungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viuongo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji;

Bali Mungu ameungamanisha mwili, kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vituzane kila kiungo na mwenziwe. Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho."

Kile ambacho Paulo anasema hapa ni muhimu sana, analosema ni kuwa kila mmoja anastahili kupewa nafasi, kukuza na kufanyia kazi kipawa chochote ambacho Mungu amepeana. Kanisa sio wale tu waliona na mwito kwa ofisi ya huduma tano, iwapo kazi ya kanisa itaenda kufanyika kama vile ambavyo Mungu amepangilia ifanyike, basi kila mtu lazima afanye nafasi yake.

Kitika Marko sura 10 msitari wa 35 hadi 44 Yesu alihitimiza hali yote kwa ukamilifu: "Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea wakamwambia, Mwalimu twataka utufanyie lolote tutakalokuomba. Akawambia mwataka ni wafanyie nini? Wakasema, utujalie sisi, tuketi mmoja mkono wako wa kuume na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.

Yesu akawambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ni nyweacho mimi au kubatzwa kwa ubatizo ni batizwao mimi? Wakamwambia twaweza. Yesu akawaambia, kikombe ni kinyweacho mimi mtakinywea, na ubatizio ni batizwao mimi mtabatizwa. Lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.

Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwa kasirikia Yakobo na Yohana. Yesu akawaita akawaambia, Mwajua yakuwa wale wanaohesabiwa kuwa wa kuu wa mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kutoa nafsi ytake iwe fidia kwa wengi."

Hii ni moja ya baadhi ya vitu muhimu katika kufaulu kwa mwili wa Kristo, kwa njia ambayo Kristo aliikusudia, iwapo hili litafanywa basi kanisa lazima liongozwe na, kujawa na watu wenye unyenyekevu.

back to main articles page